WATANZANIA NCHINI ITALY WATOA SHUKRANI KWA MH WAZIRI KWA MENGI ALIYOYAFANYA KAMA MLEZI
WU® MEDIA
ROME,ITALY 14/09/2024
Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki ameagana na Watanzania nchini Italy RASMI.
Katika hafla hiyo Diaspora kupitia viongozi wa jumuiya zao waliongea mengi ya kumshukuru Waziri,kwa jinsi walivyoishi nae Kama mlezi wao kwa kipindi cha miaka mitatu. Walisema wanajisikia furaha na fahari kwa uteuzi wa Balozi wao kwenye nafasi ya uwaziri. Diaspora walisema ni mara ya kwanza kutokea kuagana na Balozi kwa aina ya kipekee. Diaspora Italy walieleza mafanikio waliyoyapata kupitia Balozi Kombo kwa kipindi kifupi. Wameongea mengi lakini zaidi wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Dkt Samia Suluhu Hassan,na wametuma salaam kwake kuwa wanamuombea, wako pamoja nae na wanataka ajue kuwa Diaspora wana deni kwake na wakati ukifika watarudisha hisani.
Mhe.waziri amesisitiza upendo na mshikamano baina yao na kuhakikisha wanazitumia fursa mbalimbali kwa maendeleo ya nchi yao lakini kwa maendeleo yao wenyewe kwa kuwa wapo Ughaibuni kutafuta. Wengi wa diaspora walitoa machozi ya furaha lakini pia ya kutamani kuendelea kuwa nae Kama mlezi wao. Balozi Kombo ameacha alama isiyofutika kwa diaspora nchini Italy.
Mhe. Waziri wakati akiongea kwenye mahojiano na Wabongo Ughaibuni Media , ameeleza mchakato wa Hadhi Maalumu na kuwa yajayo ni mazuri. Mahojiano ya Waziri yatapatikana kwenye YouTube Channel ya Wabongo Ughaibuni Media.
GFAMILY KAGUTTA
WU® MEDIA Rome, Italy