Havana Cuba
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amesisitiza kuwa Wizara yake itaendeleza jitihada za kutafuta fursa za Lugha ya Kiswahili duniani kupitia Balozi zake nje.
Msisitizo huo umetolewa wakati akitoa salamu kwenye hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Kiswahili linalofanyika jijini Havana, Cuba na kuhudhuriwa na washiriki wapatao 400 kutoka sehemu mbalimbali duniani pamoja na wadau wa Kiswahili kutoka Tanzania.
Kongamano hili ni matokeo ya jitihada zinazofanywa na Balozi za Tanzania ikiwemo Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Cuba uliofanikisha kufanyika kwa tukio hili muhimu ambalo ni utekelezaji wa jukumu la Wizara la kubidhaisha Kiswahili duniani. Jitihada hizo zinaenda sambamba na zile zilizowezesha kutambulika kwa Kiswahili na kupewa tarehe maalum ya kuadhimishwa duniani ambayo ni tarehe 7 Julai ya kila mwaka.
‘’Kiswahili kinahitaji ushindani ili kiendelee kukua hivyo nitoe rai kwenu wataalamu na wadau wa Kiswahili kujifunza lugha nyingine ili kurahisisha zoezi la kufundisha na kusambaza Kiswahili kwa wageni. Pia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itaendele kutoa fursa za Kiswahili duniani kupitia Balozi zake, hivyo, ni jukumu la pamoja kuhakikisha fursa hizo zinatumika kikamilifu”, alisisitiza Waziri Kombo.
Vilevile, Waziri Kombo ameeleza kuwa katika kuendeleza jitihada za kukuza Kiswahili, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akihutubia kwa lugha ya Kiswahili katika mikutano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Wizara inaendelea na jitihada za kushawishi Kiswahili kitumike katika Jumuiya za Kikanda zingine ambazo Tanzania ni Mwanachama.
Waziri Kombo ametumia nafasi ya Kongamano hilo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Rais wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Miguel Díaz-Canel kwa kuimarisha na kukuza ushirikiano ulioasisiwa na waasisi wa mataifa hayo mawili.
Pamoja na masuala mengine Waziri Kombo alitoa salamu za pole kwa Serikali ya Cuba kufuatia kutokea kwa Kimbunga Rafael ambacho kimeleta athari kadhaa nchini humo. Aidha, ameishukuru nchi ya Cuba kwa ukarimu uliotolewa na nchi hiyo licha ya changamoto inazopitia.
Kufuatia kuahirishwa kwa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia SuluhuHassan nchini Cuba, ufunguzi wa Kongamano hilo ulifanywa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ambaye aliwasilisha hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hotuba ya Mhe. Rais imesisitiza umuhimu wa lugha kama nyenzo muhimu katika kurahisisha mawasiliano na kurahisisha shughuli za kiuchumi ikiwemo biashara. Katika Hotuba yake hiyo, Rais Samia ametambua mchango wa Cuba katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika na kusema kufuatia umoja na mshikamano uliopo Tanzania itaendeleza ushirikiano wake na Cuba ikiwa ni pamoja na kulaani vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba.
Naye Waziri wa Elimu ya Juu wa Cuba, Mhe. Walter Baluja Garcia aliishukuru Tanzania kwa kuiheshimisha Cuba kwa kuipa wenyeji wa Kongamano hilo, pia akaeleza katika kuendelea kukuza ushirikiano na mawasiliano kwa sasa Chuo Kikuu cha Havana kina wanafunzi 50 wa lugha ya Kiswahili.
Kongamano la Biashara na Uwekezaji Saudi Arabia
NAIBU WAZIRI LONDO AZINADI FURSA ZA KIUCHUMI NCHINI URUSI
Moscow
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo amezinadi fursa za mbalimbali za kiuchumi ikiwemo uwekezaji, biashara na utalii nchini Urusi wakati alipokutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa shirikisho la Urusi, Mhe. Bogdanov Mikhail Leonidovich.
Mazungumzo ya viongozi hao yamefanyika tarehe 10 Novemba, 2024 pembezoni mwa Mkutano wa Kwanza wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi za Afrika na Shirikisho la Urusi unaofanyika mjini Sochi, Urusi
Pamoja na mauala mengine, wamejadili kuhusu Ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Urusi tangu enzi za Baba wa Taifa Hayati, Mwl. Julius…
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Dkt. Tewodros Beleke Mkurugenzi wa Programu za Dunia na Mwakilishi wa Susan Buffet Foundation leo tarehe 11 Novemba, 2024 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
The government has proposed amendments to its laws so as to introduce a ‘special status’ to citizens of other countries with Tanzanian roots.
Tabled in Parliament on Friday, November 8, 2024, the Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No 4) Bill, 2024, amends the Immigration Act and the Land Act so as to accommodate the changes aimed at strengthening ties with the diaspora community.
The proposals aim, among other objectives, to grant Tanzanian nationals who have acquired citizenships of other countries the legal right to own property, including land, in the motherland, as well as the freedom to transfer or bequeath such assets.
The government is also seeking to ensure that Tanzanians in diaspora who hold passports of other countries are not subjected to the vigorous visa application procedures that foreign nationals go through.
The proposed amendment of the Immigration Act introduces a ‘Diaspora Tanzanite Card,’ which will be issued to non-citizen members of the Tanzanian diaspora upon receiving special status.
“A card issued in terms of this Act shall be valid for a period of ten years and may be renewed,” states the Bill in part.
The Bill explains in detail the eligibility for the status, procedure for application, conditions and things that may lead to revocation of the special status.
The Diaspora Tanzanite Card grants non-citizen Tanzanians a ‘special status,’ allowing former Tanzanian citizens and their descendants to enter, reside, and participate in economic and social activities within Tanzania.
According to the Attorney General’s office, the initiative recognises the contributions of Tanzanians abroad and aims to “foster closer ties with Tanzanians overseas.”
Source: #TheCitizenUpdates
UTEUZI
Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Kiswahili lilifanyika tarehe 8 hadi 10 Novemba, 2024 jijini Havana, Cuba.
Kongamano hilo lililofunguliwa na Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa niaba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liliwakutanisha wadau wa Kiswahili wapatao 400 kutoka Nchi mbalimbali duniani.
Maonesho ya Utalii wa Tanzania Ujerumani yafana
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mh Hassani Mwamweta ameyaeleza makampuni makubwa ya Utalii nchini Ujerumani kuwa hawatajutia kuifanya Tanzania kama chaguo namba moja la kupeleka watalii pamoja na kuwekeza kwenye utalii.
Balozi Mwamweta ameyasema hayo wakati akifungua Maonesho ya Utalii ya ‘My Tanzania Roadshow 2024’ jijini Frankfurt, Ujerumani yaliyoratibiwa na kampuni ya utalii ya KiliFair kwa kushirikina na Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) pamoja na Hifadhi ya Ngorongoro.
Ameeleza kuwa Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imejidhatiti katika kujenga mazingira rafiki kwenye Sekta ya Utalii ili kukuza utalii wa Tanzania, kuvutia uwekezaji na kukuza Soko la Utalii.
Balozi…
NAIBU WAZIRI LONDO ASISITIZA NGUVU YA PAMOJA KATIKA KUYAFIKIA MAENDELEO ENDELEVU
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo amesisitiza umuhimu wa nguvu ya pamoja katika kumaliza changamoto za kidunia na kuleta ustawi katika jamii ili kuyafikia maendeleo endelevu.
Msisitizo huo ameutoa alipokuwa akitoa salamu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo katika Mkutano wa Kwanza wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi za Afrika na Shirikisho la Urusi uliofanyika tarehe 9 hadi 10 Novemba, 2024 mjini Sochi, Urusi na kuongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho…
MABALOZI WAWAPIGA MSASA WATUMISHI WA MAMBO YA NJE
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wametakiwa kuvuna uzoefu kutoka kwa Mabalozi Wastaafu na wwbobevu ambao waliupata baada ya kutumikia nchi hii kwa uadilifu mkubwa na kusaidia kupaisha diplomasia ya Tanzania ulimwenguni.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Said Shaib Mussa wakati anafungua mafunzo ya Mawasiliano ya Kidiplomasia kwa watumishi wa Wizara yanayofanyika jijini Dodoma kwa siku tano kuanzia tarehe 11 hadi 15 Novemba 2024.
Mhe. Balozi Mussa alisema Wizara imeandaa mafunzo hayo na kuleta Mabalozi wastaafu na wabobevu kuyaendesha ili kuwajengea uwezo watumishi kuwa na ujuzi na mbinu bora za kufanya mawasiliano sahihi kwa kutumia nyen…