0 0
Read Time:41 Second

Frankfurt

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta ameyataka makampuni makubwa ya Utalii nchini Ujerumani kuifanya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama chaguo namba moja barani Afrika kwenye kuwekeza na kupeleka watalii wengi.

Balozi Mwamweta ameyasema hayo wakati akifungua Maonyesho Makubwa ya Utalii yanayofahamika kama “ My Tanzania Roadshow 2024” kwenye Jiji la Frankfurt, Ujerumani yaliyoratibiwa na Kampuni ya Utalii ya Kili Fair kwa kushirikina na TTB, TANAPA pamoja na Ngorongoro.

Pamoja na mambo mengine, ametumia fursa hiyo kueleza kuwa, Serikali ya Tanzania, chini ya uongozi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imejizatiti kutengeneza mazingira rafiki kwenye Sekta ya Utalii ili kuvutia wawekezaji kwenye sekta hiyo na kukuza Soko la Utalii wa Tanzania Bara pamoja na Zanzibar.

Aidha, Balozi alifafanua kuwa Mamlaka za Tanzania zitaendelea kutoa huduma bora kwa watalii ikiwezo huduma ya “Visa on arrival”

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %