MADA: ” Insights into Swahili literature, culture and religious practice”
Prof. Em. Farouk Mohamed Husein Tharia Topan yupo nchini Italy akiendesha warsha ya Fasihi ya lugha ya Kiswahili,Utamaduni na utendaji wa dini.
Prof. Topan anaendesha warsha hiyo kwa mualiko wa Chuo kikuu cha L’orientale kilichopo jijini Napoli. Warsha hiyo imeenza tarehe 13/11/2024 na itaendelea hadi tarehe 28/11/2024 katika kumbi za chuoni hapo Palazzo Corigliano.
Prof. Farouk Mohamed Husein Tharia Topan, Mtanzania aliyezaliwa Zanzibar ni Profesa Mstaafu katika Chuo Kikuu cha Aga Khan mjini London na mtaalamu wa fasihi ya Kiswahili na masomo ya Kiislamu akirejelea hasa eneo la Bahari ya Hindi, pamoja na mtunzi wa tamthilia tatu za Kiswahili.