
Boston
Mwanariadha nguli wa Tanzania, Alphonce Felix Simbu ameendelea kung’ara kwenye anga za kimataifa baada ya kushika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon zilizofanyika leo Jumatatu Aprili 21, 2025 na kujinyakulia zawadi ya Dola za Marekani 75,000, sawa na Sh201.4 milioni.
Simbu ambaye ameendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania alikimbia kilomita 42 na kumaliza mbio hizo kwa muda wa saa 2:05:04 katika mashindano hayo yaliyohusisha wanariadha mahiri kutoka mataifa mbalimbali.
Simbu ambaye alikuwa miongoni mwa washiriki 10 waliopata mwaliko maalum kushiriki kutokana na rekodi yake nzuri katika mashindano ya kimataifa amewapiku wanariadha wengi waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda.
Mkenya John Korir ametwaa ushindi kwa kutumia muda wa saa 2:04:45, na kufanikiwa kuchukua zawadi ya Dola 150,000, sawa na Sh403.2 milioni.