0 0
Read Time:3 Minute, 36 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
August 3,2021.

Wakati wa wimbi la Kwanza la uviko -19 duniani,Rais hayati John Pombe Magufuli, alikataa kuiingiza Nchi katika kitu kinaitwa lockdown lakini angalau yeye alikuwa na msimamo wa wazi unaoeleweka lakini leo hii watanzania bila kujua,tunaweza kuwa tupo kwenye lockdown kali zaidi kuliko ile tuliyoikataa mwaka jana!

Hiari yazidi utumwa lakini sio kila hiari ni Uhuru wa maisha lakini kuna utumwa mwingine unaweza ukaupractice leo lakini ukakusaidia kuokoa maisha yako na familia yako!

Juzi nilistuka mno baada ya kupewa taarifa kuhusu kifo cha kijana mdogo kabisa mjini hapa Mbeya!kijana alikuwa na ndoto nyingi za kwake binafsi na familia lakini juzi ndoto hizo zimekatika gafla na wala hatoiona tena familia yake ya watoto wawili,hatomwona tena mke wake mrembo,hatoiona tena gari yake aina ya Harriar High bred!

Ndio kashaondoka na uviko -19 lakini bado hatushtuki wakati mifukoni mwetu hatuna hata barakoa,mifukoni mwetu hatuna hata santaiza na wala hatujanawa walau mikono tu tangu tulivyokunywa chai ya asubuhi,hivi Watanzania nani katuroga?nani atakuja kutufungua minyororo hii ya utumwa wa akili?

Tumekuwa sawa na kuku wa kisasa yule wa bandani ambaye nae pia anaamini kuwa yupo huru kisa yupo anatembea tembea ndani ya kuta nne za banda lake lakini kiukweli kuku huyu hayupo huru kwani uhuru wake uishia ndani ya kuta nne za banda lake tu!

KWANINI NASEMA WATANZANIA LAZIMA TUJITOE KWA LOCKDOWN HII SASA?

Kuna sababu kadha wa kadha ambazo zinaonyesha tupo kwenye lockdown tena mbaya zaidi ya jana lakini kibaya zaidi hatuchukui tahadhari yoyote ya maana ambayo angalau wakati wa wimbi la mara ya kwanza la uviko -19 tulikuwa tunachukua!This time not!

1.Mpaka sasa akili za Watanzania zipo kwenye lockdown mbaya zaidi ya ile ya Jana!sijui kama tunajua hilo!Kitendo cha kukataa kufungua masikio yetu na kuamua kusikiliza “selective bad news” kuhusu ugonjwa wa Corona kinatuweka kwenye risk kubwa zaidi”Prandemic dillema”.

Kwangu mimi,hii ndio lockdown mbaya zaidi ya kuwa na “selective exposure news” na kukataa kusikiliza realities zingine kuhusu uviko 19 zinazoendelea duniani!Zaidi ya watu 90,000 walikuwa juzi kati katika fainali ya EURO pale Ulaya bila kuvaa barakoa wala bila distancing kwa sababu tu walishapata chanjo ya uviko 19.Habari hii akili zetu zimeikataa kabisa wakati wote tulikuwa kwa TV tukiangalia mpira pendwa wa ulaya!

2.Kwa sasa,almost asilimia karibia 90 ya Watanzania hawana sifa ya kuchanganyika na wenzao duniani kwa kutoka nje ya mipaka kwa sababu ya kukosa “global criteria” za kujikinga na uviko 19.Yaani kwa sasa Watanzania wapo kama yule “kuku wa kisasa bandani”ambaye anajidanganya yupo huru kwa sababu ya kutembea ndani ya zile kuta nne na nje ya hapo hawezi kuwa huru!”Mind lockdown”.

3.Baya zaidi hata yule Mungu tuliyemlilia na mpaka akatusikia last time hatajwi tena na Watanzania wengi makanisani wala misikitini!Je,tutapona na nini wakati watu wanendelea kufa mitaani?,je,tutapona kwa kukataa chanjo ya uviko 19 pekee yake?

Watanzania this time naweza kusema hawana “base” yoyote ambayo they stand for kuhusu kuzuia maambukizi ya uviko 19!Hawamtaji Mungu tena,hawataji science tena wala hawataji mitishamba “nyungu” tena zaidi wanataja ubaya wa chanjo ya uviko 19 tu.

4.Wale waliosoma historia ya “Working Class Movement” pale uwingereza miaka ya mapinduzi ya viwanda watakumbuka jinsi ambavyo “Wazungu vichaa” kupitia “Ludists” au “Luddism movement” walivyoangaika na kuharibu mashine ndani ya viwanda wakidhani ndio adui wa ajira zao!

Watanzania hawa mpaka leo hawamjui adui yao,wengi wanadhani adui wa maisha yao kwa sasa ni chanjo ya uviko -19 kumbe adui yao namba moja ni uviko mwenyewe!Watanzania wanaogopa chanjo kuliko uviko 19,hatari!

Wanajeshi wanasema “failure to identify the real enermy at war ,it is an half defeat”!Tukubali kuwa Watanzania for far tunapigwa na uviko 19 kila siku huku mitaani lakini bahati mbaya hatumwogopi anayetuua lakini tunamwogopa chanjo!

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliwahi kusema”…..akili za kuambiwa changanya na akili za kwako then amua” maisha yako!Nenda kachanje kwani chanjo ya uviko 19 ni maisha yako ya leo na kesho!

Mwandishi ni kijana wa CCM,Makamu wa Rais wa zamani,Serikali ya Wanafunzi Daruso-IJMC,Mhadhiri Msaidizi wa zamani Vyuo Vikuu vya Saut & Tumaini,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari -Maelezo,Ofisa kadeti wa zamani,Chuo cha maofisa wa Jeshi Monduli Arusha na Mtia nia wa Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %