
JUMUIYA YA WATANZANIA KOREA. TANROK
Umoja wa Watanzania waishio Korea (TANROK) hivi karibuni walichagua viongozi wa kuiongoza Jumuiya hiyo katika Mkutano Mkuu uliofanyika kwa njia ya Mtandao.
Pichani ni Mwenyekiti Mpya wa TANROK Bw. Robin Noel Damas (Wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi Bw. Deogratius Mwanyasi (Aliye katikati)na Mlezi wa Diaspora, Bw. John Masuka. Wa pili kulia ni Mweka Hazina Bi. Elizabeth Mgimba na wa pili kutoka kushoto ni Mch. Daniel Seni, katibu wa Jumuiya hiyo.
Hafla ya makabidhiano ya Uongozi ilifanyika tarehe 11 Septemba 2021 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ubalozi wa Tanzania, Korea. Tunawapa hongera sana na kuwatakia kazi njema.










