0 0
Read Time:2 Minute, 52 Second
jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
November 7,2021.

Kuna imani katika Afrika kuwa madini hasa Dhahabu yanahusishwa na imani za kishirikina na baadhi ya watu wanasema dhahabu inaweza kupotea katika mazingira ya kutatanisha!kwahiyo kama kuna ukweli katika hilo ndio maana viongozi wengi wanaonekana kurogwa na madini haya!

Inasemekana,Ufaransa ndio nchi ya nne duniani kwa kuwa na akiba kubwa ya Dhahabu “World Gold Reserve” kwa tani ya dhahabu karibia 2436 yenye thamani ya karibia dola za kimarekani 111.8 Billion wakati haina hata mgodi mmoja wa dhahabu ndani ya “territory” yake yenyewe!

Nchi ya Mali,haina hata akiba ya Dhahabu wakati ina migodi ya dhahabu karibia 860 na uzalisha tani karibia 50 kila mwezi.

Kuonyesha kuwa BOT walikuwa kwenye usingizi mkubwa huko nyuma,Mh Rais Samia Suluhu Hassan aliagiza BOT kuanza kununua dhahabu safi kama njia ya kulinda akiba ya Nchi kwahiyo ni wazi kuwa BOT walikuwa either wanafanya au hawafanyi ipasafyo!,Hii ni kwa mujibu wa Jarida la Extractive Baraza la June 15,2021.

Wakati March 2021 Tanzania ilikuwa ikishangilia kuongezeka kwa mauzo ya nje ya dhahabu kwa dola za kimarekani 240.4 wenzetu wafaransa walikuwa wanashangilia kujaza kibubu chao cha dhahabu bila hata kuwa na mgodi mmoja wa dhahabu wa ndani ya Nchi yao!

Hivi diplomasia ya uchumi ya Tanzania bado haijatambua Nchi dhaifu huko duniani na kwenda “kupora”utajiri wao?.
Vyombo vyetu vya “stratejia” ya uchumi,ulinzi,usalama bado havina njaa ya kufanya Tanzania kuwa Nchi kubwa?,unawezaje kuwa mkubwa wakati mpaka leo hatuna “reserve” ya kutosha ya diamond,copper,coal,na mengine mengi!

Je,ile Nikel ya kabanga tuna mpango gani wa kuiwekea “reserve” kama Nchi!?Prof Luoga unaweza ukatumbia una mipango gani ya kutengeneza “Banki ya rasilimali madini” ndani ya BOT ambayo itakuwa na akiba ya kutosha kwa kila madini yanayochimbwa hapa ndani!lazima tuanze kuwaza haya!”Resource Nationalism”.

Kwanini tafsiri yetu ya diplomasia ya uchumi inakuwa na mtazamo “narrow” sana kiasi kwamba mpaka leo tunaamini kuwa uwekezaji”FDI’s” ndio zitatutoa!Kwanini hatufikiri kuiwezesha Stamico kwenda Congo,Mali,Senegal kwenda kuvuna utajiri wa madini?

Tunashindwaje kumpa majukumu maalum kampuni yetu ya kizalendo ya Stamico na tukajaza “majasusi uchumi” wetu huko na kuwatuma nje ya mipaka kwenda yetu kupora utajiri katika Nchi dhaifu?Nani katudanganya kuwa tunaweza kuwa Taifa kubwa kwa “kuitisha” wewekezaji kutoka nje?,Inasikitisha kidogo kuona uongozi wetu haupo aggressive katika masuala ya msingi ya ujenzi wa Taifa bora la kesho,Tanzania ya kesho iliyo imara zaidi kuliko ya leo!

Wakati hivi karibuni kunatajwa kuwepo kwa kongamano la diplomasia ya uchumi ya Tanzania, Je, washiriki wetu wa kongamano hilo kama maprofesa na madokta wana mawazo haya?au nao pia wanawaza kuhusu kuchochea uwekezaji tu?kama ni hivyo basi tupo kwenye mkwamo mkubwa mno!

Ukitaka kuwa Taifa kubwa lazima ufikilie makubwa regardless ya uwezo wako!kuwa Taifa kubwa unahitaji mambo makubwa matatu;(i)ujeuri wa kutaka na kuamini kuwa unaweza kuwa Taifa kubwa (ii)wivu wa kutaka kuwa Taifa kubwa(iii)uthubutu wa kutaka kuwa Taifa kubwa kwa maana unafanya mambo gani yasiyo ya kawaida ya kukufanya kuwa Taifa kubwa.

Kama hatuwezi kufanya haya basi tutaendelea kuwa Taifa “chumia tumbo” miaka nenda rudi,inauma sana kwani uwezo huo tunao,why not now?

Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani Vyuo Vikuu vya Saut & Tumaini Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %