0 0
Read Time:57 Second

Mabalozi wa Tanzania wafunguka kuhusu fursa za kiuchumi Ulaya

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na watu wake wana nafasi kubwa ya kuzitumia fursa za kiuchumi zilizopo nchi za Bara la Ulaya kunufaika kiuchumi, kutokana na misingi mizuri ya uimarishaji wa diplomasia ya uchumi iliyowekwa na Serikali.

Hayo yamesemwa kwa nyakati toafauti leo Agosti 10, 2022 na watoa mada ambao ni wanadiplomasia wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mataifa mbalimbali barani Ulaya.
Mkutano huu ulioratibiwa na Watch Tanzania kupitia Mtandao wa Zoom uliangazia hasa juu ya KUKUA KWA DIPLOMASIA YA UCHUMI NA FURSA ZA KIUCHUMI ZINAZOPATIKANA NCHI ZA BARA LA ULAYA.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dr Asha Rose Migiro amesema; Uingereza imekuwa mshirika mkubwa sana wa maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania, kwani imeweza kusaidia kwa kushirikiana na Serikali kukamilika kwa miradi mbalimbali ikiwemo ya sekta ya ujenzi, kilimo, ufugaji ,Sayansi na Teknolojia.

Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh Grace Alfred Olotu na amesema; Sweden ina miradi nchini Tanzania isiyopungua 200 kutoka makapuni mbalimbali, miradi hiyo ina thamani ya dola za Kimarekani milioni 726.63 na inachangia ajira za moja kwa moja zipatazo 15,191;

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %