
Huyu ndiye mwenye Mzizima yake sasa
Anaitwa mzee Jumbe wa Tambaza, ambaye zama za kale kabla ya kuwepo kwa Dar es Salaam, alikuwa mmiliki wa eneo lote lililoitwa Mzizma.
Yani kuanzia kule Magogoni, Ikulu, hadi Daraja la Salenda (Selander Bridge), njoo Upanga kule shule ya Tambaza hadi Makao Makuu ya Jeshi, nenda hadi Kisutu kisha ingia Uhindini yote na Posta yake, yote ilikuwa miliki yake halali.
Miaka ya 1860s, alilimega eneo hilo kuanzia Magogoni hadi Salenda na kumuuzia Sultan Majid wa Zanzibar ambaye alitumia eneo hilo kujenda majengo ya chuo Kikuu cha Kiislamu cha Daru Salaam (hivi sasa Ikulu) na hostel zake ambazo sasa ni Hospital ya Saratani ya Ocean Road.
Zama za miliki ya mzee Jumbe wa Tambaza, eneo lile la Magogoni hadi Salenda lilijulikana kama Mzizima kutokana na utulivu wake pamoja na wanyama wakali waliokuwepo. Ikawa kila aliyepita eneo hilo lazima mwili wake uzizime.
Eneo lake jingine, ukiingia huku Barabara ya Bibi Titi hadi Kisutu na kuja huku kwetu Kariakoo, liliitwa Tindwa na ndio ulikuwa mji haswa wenye wakazi kama mia sita (600) hivi.
Kusanyiko wa eneo lake la Tindwa, alilouza na jingine kuligawa bure tu na kugawa, na miji ya Kunduchi na Mbwa Maji, ndio iliyounda Jiji la Dar es Salaam hii ya sasa ambayo:
Jina hili la Dar es Salaam lilibadilishwa na Wajerumani toka jina la Daru Salaam lililotokana na jina asili la Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Daru Salaam chuo ambacho baadae Wajerumani walilifanya kama Ikulu baada ya kusafirisha Waislamu kimabavu miaka ya 1870s.
Imeandaliwa na Mosses Ismail wa Wa-mission Quarter Kariakoo








