0 0
Read Time:3 Minute, 16 Second
Jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,MBEYA.
Octoba 28,2021.

Ukitaka”kumbomoa” hayati John Pombe Magufuli lazima kwanza uwe na mambo makubwa matatu(i)Ukichaaa(ii)akili nyingi au(iii)utafiti wa kisayansi sana,Nje ya hapo “utabomoka” mwenyewe.

Rais wangu na Mama yangu,Mh. Samia Suluhu Hassan juzi amesema,Nanukuu”…viatu vya JPM ni vikubwa mno kwake…”,japo hii inaweza isiwe nukuu rasmi sana!

Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mzee Ally Hassan Mwinyi pia aliwahi kukiri pale Dodoma,Nanukuu…”…na sisi tulifanya lakini huyu kafanya pakubwa….”yaani JPM.

Rais wa awamu ya Nne Mzee wangu Jakaya Kikwete aliwahi kusema kitu kuhusu hayati Magufuli,Nanukuu…”…mwenzetu katuzidi uthubutu ..lakini suala la kuamia Dodoma ni mpango wa CCM wa miaka mingi…..”.

Ni wazi kuwa unahitaji “ukichaa” wa kiwango cha juu kupingana na maneno ya viongozi hawa wa kitaifa kuhusu mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano ya CCM chini ya hayati JPM na Mama Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka yao mitano.

HAKUNA kipindi chochote ndani ya miaka ishirini nyuma ambapo CCM ilikuwa na ushawishi mkubwa kwa vijana wa kitanzania kama wakati wa hayati JPM!HAKUNA wakati wowote ambapo vijana walijivunia kuvaa kombati ya CCM kama wakati wa hayati JPM na makamu wake Samia Suluhu Hassan!

CCM yangu inahitaji tafakuri pana sasa, kupima kama kweli ule ushawishi wetu kwa vijana wa kitanzania kama bado tunao na kama hatuna basi tunapaswa kuhusaka kwa gharama yoyote kuelekea mwaka 2025.

HOJA YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO YA JPM KUKOPA KWA “FUJO”.

Kwa mujibu wa andiko la Ndugu Balile kwamba Serikali ya awamu ya tano ndio Serikali ambayo inaongoza kwa kufuja fedha kupitia mikopo ya nje kuliko Serikali zote za Tanzania!

Je,KUKOPA ni dhambi?je,kukopa ni aibu?unakopa hili ufanye nini?nadhani hili ndio swali la msingi kuliko kutaja kiasi gani umekopa!

1.Mradi wa SGR ya Kenya kwa mujibu wa Jarida la “The Africa Report” la January 22,2021 linasema”…..when payments are scheduled to began for a USD 1.4 Billion loan from China Exim Bank for Nairobi -Naivasha section….”.Kumbe huko duniani kila mtu anakopa!Ishu ni je,unakopa kwa sababu zipi na sio kiasi gani!

Hayati JPM aliweza kutandika reli ya SGR ya viwango vya juu kabisa kuliko reli ya Kenya hivyo kutufanya Tanzania tuje kuwa na reli bora katika Afrika!

2.Serikali ya CCM ya awamu ya tano,chini ya JPM na Samia Suluhu Hassan iliweza kuvunja rekodi ya kuingia katika uchumi wa kati kabla ya muda uliopangwa yaani 2025.Hii ina maana gani?Mikopo ambayo Ndugu Balile ameitaja kwamba inabebesha mzigo Taifa leo,ina mahusiano ya moja kwa moja na Nchi kuingia katika uchumi wa kati!

Inahitaji shule na akili kubwa Ndugu yangu Balile kujua maarifa haya!Serikali ya awamu ya tano ndio labda inaweza kusemwa vibaya zaidi na watumishi wa Umma kwa “Ukuda” na kwa kubana matumizi ya Serikali!Unahitaji uwe kichaa wa viwango vya juu kuyakataa haya!

3.Haijawahi kutokea!Serikali ya CCM ya awamu ya tano chini ya hayati JPM na Mama Samia Suluhu Hassan aliweza kujenga vituo vya afya vingi zaidi ndani ya miaka mitano kuliko vilivyowahi kujengwa tangia Uhuru wa Tanzania!

Waziri wa sasa Muungano na Mazingira kaka yangu Suleman Jaffo, anaweza akawa shahidi mzuri wa kitakwimu!

Niseme mangapi?ndio maana nikasema,unahitaji kuwa na mambo makubwa matatu kabla ya kutaka kubomoa kazi takatifu za Serikali ya awamu ya tano ya hayati JPM na Samia Suluhu Hassan!

.
“…ukichaaa,akili nyingi au utafiti wa kisayansi….”.

Tukubali tu kuwa yoyote anaweza kumtaja hayati JPM kwa sababu hizo kuu tatu!Bahati mbaya Ndugu Mwanajukwa la Habari,Basile sijui anaangukia wapi katika sababu kuu hizo tatu!

Mwandishi ni kijana wa CCM,Makamu Rais wa zamani Daruso-IJMC,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli,Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Saut &Tumaini University,Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255746726484.
+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %