0 0
Read Time:2 Minute, 20 Second

Na Dr Yahya Msangi

Mama haya ndio yataleta kitimtim kwenye haya majadiliano:

 1. Héla (eeeela)
  Toka Obama na wenzie waahidi bilioni 100 mwaka 2015 pale Copenhagen mpaka dakika hii wametoa bilioni 70 tu! Na wamekula wenyewe bilioni 40 Kati ya walizotoa. Mama héla hii sio ombi ni wajibu wao. Sao ndio wamwemwaga hewa chafu angani joto likaongezeka kwa 1 centigrade ! Naam! Kizaazaa chore hiki ni 9ngezeko la dégrée 1 tu kutokea 1900! Sasa ukifika 2030 hivihivi litaongezeka tena kwa nyuzijoto 0.5 yaani itakuwa ongezeko la 1.5 tokea 1900! Tutakoma. Hatuombi HII héla Bali ni déni! Dawa ya déni si kulilipa?
 2. Ahadi feki za kupunguza kuzalisha hewa chafu. Katika mkataba wa Paris (Paris Agreement) WA 2015 Ilichukua majadiliano miaka 21 kukubaliana! Wakaahidi watapunguza kwa asilimia 50 (50%) uzalishaji hewa chafu. Fiksi tu! Aliyejitahidi saaana kafikia asilimia 25 (25%) tu! Bora n’a Trump alikuwa muwazi akakataa mkataba!
 3. Teknolojia
  Mama mkataba unawataka watupe teknolojia bila malipo au kwa gharama nafuu. Pia unawataka watujengee uwezo ndani ya nchi zetu tuzalishe teknolojia wenyewe. Nayo fiksi tu. Tumeishia kupewa majiko yasiyotumia mkaa kwa wingi. Tumeishia kupiga marufuku mifuko ya Rambo! Na tunakenua! Kwa kuwa wao ndiyo chanzo cha tatizo wanawajibika na hili. Sio ombi.
 4. Fair Play
  NCHi zetu ambazo hazisababishi tatizo zinatakiwa zichukue hatua Sawa na wahalifu. Mwaka 1992 kwenye mikutano wa kwanza (Earth Summit) Mjini Rio De Janeiro jamii ya kitaifa yoote iliridhia kanuni inaitwa “THE PRINCIPLE OF COMMON BUT DIFFERENTIATED RESPONSIBILITY” kifupi CBDR. KANUNI hii inamaanisha hivi – tatizo ni letu wote lakini kuna wenye wajibu zaidi ya Wengine! Lakini Sasa kinyume na kanuni hii wakubwa wamelazimisha nchi zetu nazo zipunguze kuzalisha hewa chafu kama wao! Na kwa Ujinga au uroho wa wawakilishi wetu walikubali!
  Ni kituko mama! Afrika nziima inachangia only 4% ya hewa chafu duniani! Na asilimia 90 ya hiyo asilimia 4 inatoka Afrika Kusini na Nigeria tu! Yaani Wengine wooote 53 ikiwemo Tanzania tunachangia asilimia 10 tu ya hiyoo asilimia 4! Maana yake Kila nchi inachangia 0.0000007% duniani! Utapunguza Nini? Upunguze usichokuwa nacho? Sawa Mwenye ugali sufuria mzima amtake Mwenye tonge aweke akiba ya ugali!

Mama yapo mengi lakini haya manne hebu wapige nayo. Wataalamu wetu wasikuandikie hotuba ya kuidhinisha huu uhalifu wa Kimataifa!

Mwisho kabisa chunguza sifa za watakaotuwakilisha Glascow. Tuna historia mbaya sana sisi waafrika kwenye ushiriki. Tuna wawakilishi wa ajabu sana mara nyingi. Sitaki nitaje mtu lakini pitia TAARIFA ya waliotuwakilisha India wakati wa mkutano wa 14 UNCCD mwaka 2019. Mmoja na ndiye alikuwa mkuu wa msafara alitufedhesha mnoo. Chapombe! Ilitulazimu kumuondoa ukumbini tusiingie aibu kama taïfa. Yupo ofisi ya makamu wa RAISI Mazingira. Huyo kama yumo kata fasta! Ukinijia chemba ntakutajia.

KARIBU sana Scotland. Ikikupendeza tembelea Edinburg University UONE walivyomheshimu Julius! Pia ikukupendeza andaa party ya vipapatio kwa watanzania tunaoshiriki hapa tubadilishane Mawazo. Tukilapo hamna ubaya ni wananchi wa île jamhuri!

Bon Voyage ta Excellence

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %