WAJIBU WETU VIJANA WA CCM KWA SERIKALI YETU HATUJAUTIMIZA VIZURI.
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
November 5,2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Samia Suluhu Hassan, aliwahi kusema haya alipokuwa akiongea na wahariri wa vyombo vya habari Nchini, japo maneno yangu yanaweza yasiwe exactly na yake lakini bado yatabeba maana ile ile na hapa nanukuu;
“…..unakuta mtu kuanzia mwanzo mpaka mwisho anapondaa wewee…ukadhani hana Mama huko kwao….mimi sikatai kukosolewa lakini unapokosoa niambie fanya hivi fanya vile…..”.
Mh.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Ally Mwinyi ,juzi pia alinukuliwa akiongelea kuhusu tabia inayoanza kuenea ya kusifia viongozi wa kitaifa kwa lengo la kupata maslahi fulani na hapa nanukuu;
“….Mimi napenda mtu anayeniambia ukweli kuwa hapa umekosea….sababu unaweza kujua wapi unakosea…kuliko mtu anakusifia tuu…wakati mwingine mtu anakusifia ili apate kitu fulani kutoka kwako…..”.
Katika siasa za kisasa za ushindani, vijana wa CCM lazima tubadilike katika kupambana na wapinzani wetu kwa kutumia njia za kisomi zaidi kwa lengo la kuweza kuzifunika hoja zao kwani tukifanya kama wao tutakuwa hatuleti utofauti wowote baina yetu!
Sababu sisi ni Chama dola basi tunapaswa kuwa juu ya vijana wa upinzani katika kila eneo;fikra,maono,hoja,mbinu,ukweli,matendo na hata ustaarabu wetu.Sisi lazima tutoke katika level zao za kuponda Serikali na huku sisi tukisifia Serikali yetu!
UHALALI WETU KWA TAIFA LETU UTAPATIKANA KWA KUFANYA MAMBO HAYA HAPA!
1.Kwa vijana wa CCM wajibu wetu wa kwanza lazima tuwe “Whistleblowers”dhidi ya Serikali yetu wenyewe na Chama.Sisi tunapaswa kunusa mambo mbalimbali na changamoto mbalimbali na kuzileta kwenye paltform sahihi na kuishauri Serikali yetu jinsi ya kufanya.Tunazo platforms zetu za kujadiliana mambo yetu ambazo wote tunazijua!
Sisi tunapaswa kusema lakini kwa adabu kubwa kuhusu hoja na changamoto mbalimbali za kitaifa kama njia bora ya kuisimamia Serikali yetu ya CCM!Bila kufanya hivyo tutawapa vijana wa upinzani uwanja wa kuiponda Serikali yetu bila sababu za msingi.
2.Vijana wa CCM lazima pia tuwe “magate keepers”, kwa maana kwamba lazima tuhakikishe tunajibu upotoshaji wowote unataka kufanywa na mtu yoyote au vyama vya upinzani dhidi ya Serikali ya CCM.
Dhana ya “Gate Keeping” ina maana kuwa,vijana wa CCM kamwe tusikubali jamii ya Watanzania walishwe “matango pori” na mtu yoyote au vijana wa upinzani bila sisi kusema ukweli kuhusu hoja husika kwa kuhakikisha tunajibu hoja zao kwa tafiti,takwimu na utaalam wa kiwango cha juu kwa kila hoja yenye lengo la kupotosha ukweli kuhusu Serikali ya CCM.
3.Vijana wa CCM tuna wajibu wa kuwa “Mobilizers”!Jukumu letu kubwa kuliko majukumu yote ni kuhakikisha tunawaunganisha vijana na watanzania kwa ujumla bila kujali itikadi zao, dini zao,vyama vyao na hata ukanda wao.
Wajibu wa “Social Mobilization” unaenda pamoja na kuwakumbusha Watanzania kufanya kazi kwa bidii,kuilinda amani ya Nchi yetu,kudumisha undugu,kudumisha umoja wa kitaifa kama njia bora ya kifikia maendeleo ya Taifa letu!
Lazima vijana wa CCM tukemee kwa nguvu zetu zote matukio yote yanayoweza kuhatarisha amani ya Taifa kama kutengeneza ugaidi,kupambana na vyombo vya dola na kufanya vurugu kama njia ya kuonyesha kutokukubaliana na mipango ya Serikali.
Tunaweza na lazima tuanze kujitofautisha nao kwa kufanya haya kwa kufanya hivyo tunaweza kupata heshima zaidi mbele ya jamii ya watanzania kuliko ilivyo hivi sasa ambapo tumeshindwa kuonyesha tofauti kati ya sisi washika dola na wao watafuta dola!
Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,vyuo vikuu vya Saut & Tumaini Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.
+255784159968.