Na Zain Diaspora USA
URAIA PACHA NA WATOTO
Wengi hawapangi kufeli, wanafeli kupanga!
Tunajua wewe jua limeshazama hutoboi tena, hata maana ya security clearance unaweza usiijue.
Kwa wale wanaosema wanataka watoto wao wawe na maisha mazuri kwa kupitia uraia pacha, wajifunze kitu hapa.
Wanafunzi wengi wanakuja Marekani wanapata madigrii ya IT na kadhalika lakini wanashindwa kupata kazi za maana hasa serikalini kwa sababu hawawezi kupata security clearance.
Sheria inasema mwenye uraia pacha ana uhalali wa kupata hizo kazi, lakini wanaotoa hizo security clearance wanawafelisha kwa sababu ya uraia pacha wao.
Sasa wewe kama umepanga kumzuia mwanao asifike mbali kwenye kazi za kitaaluma endelea kupigania apate uraia pacha.
Jasho litamtoka akikosa kazi ya maana huku nje kwa sababu ya uraia pacha, na huko Tanzania nako hilo shamba ulilomuandalia akute limenunuliwa na tajiri mwenye uraia pacha kutoka Kenya.
Inaitwa ugali moto, mboga moto.
Kwa sababu huwa mnaelewa vitu mkiambiwa na mzungu, nimewawekea mzungu huyo.
Msikilizeni!