1 0
Read Time:1 Minute, 34 Second

Na Mwandishi wetu

Napoli, Italy WMEDIA

Passport

Ubalozi wa Tanzania nchini Italy umeendelea na zoezi la kukabidhi passport kwa Watanzania katika maeneo ya uwakilishi wake.

Mh. S. Nnembuka akimkabidhi Mtanzania passport

Baada ya zoezi kama hilo kukamilika nchini Greece sasa pia limekamilika jijini Napoli Italy. Balozi wa Tanzania nchini Italy Mh. Mahmoud Thabit Kombo ameendelea kutimiza moja ya ahadi zake kwa diaspora tangu afike nchini Italy. Pamoja na changamoto nyingi hili la passport aliamua kulifuatilia mwenyewe mpaka kufanikisha. Haikuwa jambo rahisi kwani ilimlazimu kufanyakazi ya ziada mpaka kukubaliwa ombi lake. Katika mchakato huo Wizara ikishirikina na wenzao wa uhamiaji waliweza kutuma maofisa wa uhamiaji waliokuja katika maeneo ya uwakilishi wa balozi Mahmoud Thabit Kombo na kufanya zoezi la kupokea maombi ya passport pamoja na uhakiki wa waombaji. Watanzania kwa kauli zao walitamka kupongeza kazi iliyofanywa na maofisa hao wabobezi kwa weledi mkubwa na kuweza kusikiliza kila mtu aliyefanya maombi, pamoja na watanzania kumpongeza balozi wao lakini kwa namna ya pekee walimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali kwa namna ya pekee sana.

Siku ya alhamisi tarehe 11/05/2023, Mkuu wa kitengo cha passport na diaspora Mh. Sigfred Nnembuka akiongozana na afisa mwenzie wa ubalozi Dada Eva , walifika mjini Napoli na kukabidhi passport kwa watanzania waliokuwa na shauku kubwa ya kupata hati hiyo muhimu ya kusafiria. Mh. Nnembuka aliwatuliza wale wote ambao passport zao bado hazijafika kuwa kazi inaendelea na mara zitakapokuwa tayari watajulishwa.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania IN CAMPANIA Madam Judith Joseph , kwa niaba ya jumuiya na uongozi alimshukuru Mh. Nnembuka na kutuma salamu za shukrani kwa Mh Balozi kwa kendelea kuwasaidia na kuwajali hasa katika kupatia majawabu changamoto mbalimbali za watanzania.

Zoezi la kukabidhi passport lilifanyika katika ofisi mpya ya jumuiya ya Watanzania Italia IN CAMPANIA, Mtaa wa: Via Sant’Anna Alle Paludi 19, 80142 Napoli NA.

Picha na HJ Napoli – WU®MEDIA

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %