
WU®MEDIA
Kijana wa Kiume wa Muhamasishaji Bongozozo aitwae Mickey Reynolds (18) ameibuka Mshindi wa kwanza wa mashindano ya “Karlovac Mile” yaliyofanyika nchini Croatia ambapo amewashinda Washiriki wengine 126.
Mickey ameshinda mbio hizo za maili moja kwa kuwashinda Washiriki wengine kutoka Mataifa mbalimbali ikiwemo Croatia baada ya kufanikiwa kukimbia maili moja kwa kutumia dakika 4 na sekunde 56.
Mickey ameshiriki mashindano hayo akiwa amejisajili kama Mtanzania ambalo ni Taifa la Mama yake na baada ya ushindi alishangilia akiwa na bendera ya Tanzania.
Karlovac Mile ni Mashindano ya riadha yanayofanyika kila mwaka katika mji wa Karlovac nchini Croatia na yanatambuliwa na Shirikisho la riadha Duniani (World Athletics Organization) huu ukiwa ni mwaka wake wa 12 kufanyika mashindano hayo.










